.

.

Jumamosi, 24 Desemba 2016

G-Maker: Nimemgharamia Sholo Mwamba Kwa Mil. 40

gmaker-1Meneja wa Man Fongo, G – Maker ambaye pia ni meneja wa staa wa Ngoma ya Hunakulaga Sholo Mwamba, akifanya mahojiano leo katika Ofisi ya Global Publishers, Bamaga – Mwenge, Dar.
gmaker-2gmaker-3 Mahojiano yakiendelea.
G – Maker ambaye pia ni meneja wa staa wa Ngoma ya Hakunaga kwa mara ya kwanza amefungukia gharama alizotumia kumtengeneza staa Singeli, Sholo Mwamba kuwa ni zaidi ya shilingi milioni 40.
Akizungumza na Global TV Online kupitia kipindi cha Exclusive, G Maker alisema kuwa anajivunia kuwa na Man Fongo kwani ndani ya kipindi kifupi amepata mafanikio makubwa.
“Najivunia kwa Man Fongo. Nilikuwa nawameneji pamoja na Sholo Mwamba na niseme tu hadi sasa siwezi kumdai chochote lakini tangu nianze naye kumshepu kuwa staa hadi hapo alipo imenikosti zaidi ya milioni 40.
“Kwanza nilimkuta katika mazingira magumu, ikanibidi kumtengeneza kisaikolojia hadi kuwa katika hali ya kawaida na kuwa staa anayekubalika katika muziki wa Singeli jambo nililofanikiwa kwa asilimia kubwa japokuwa baadaye alikuja kutaka kuondoka nikamruhusu,” alisema G-Maker.