.

.

Jumamosi, 8 Oktoba 2016

Kauli ya BMT kuhusu Yanga kukodiwa kwa miaka 10


Baraza la michezo Tanzania BMT Jana October 7 2016  limetangaza msimamo
wake ikiwa ni siku moja imepita toka klabu ya Dar es Salaam Young Africans 
iweke wazi mkataba wake wa kukodiwa na kampuni ya Yanga Yetu Limited,
 Yanga ilitangaza Juzi October 6 mkataba walioingia na Yanga Yetu Limited
Septemba 2016. Baraza la michezo leo limetangaza kutoutambua mkataba huo
 wa Yanga ambao Yanga Yetu Limited waliingia na klabu ya Yanga kupitia kwa bodi 
yawadhamini wa Yanga, katibu mkuu wa BMT Mohamed Kiganja amesema kuwa
bodi ya wadhamini wa Yanga ni ya mpito na sio sawa kufanya maamuzi ya kuikodisha timu.