.

.

Ijumaa, 30 Septemba 2016

Ushindi wa Genk ya Samatta uliowafanya waongoze Kundi F Europa League


Usiku wa Septemba 29 2016 klabu ya KRC Genk inayochezewa na
nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Mbwana Samatta
ilishuka uwanjani kucheza mchezo wake wa pili wa Kundi F wa
Europa League dhidi ya Sassuolo ya ItaliaGenkwaliwakaribisha
Sassuolo katika uwanja wao wa nyumbani wakiwa na kumbukumbu ya
kufungwa mchezo wao wa kwanza dhidi ya Rapid Wien.
Katika mchezo huo ambao KRC Genk waliingia kwa dhamira moja tu ya
kupata point tatu, ulimalizika kwa KRC Genk kuibuka na ushindi mnono
wa magoli 3-1, magoli ambayo yalifungwa na Nikolaos Karelis
dakika ya 8, mjamaica Leon Bailey dakika ya 25 naThomas Buffel 
dakika ya 61 wakati Sassuolo waliishia goli moja lililofungwa na
Matteo Politano dakika ya 65.
Mtanzania Mbwana Samatta ambaye alikuwa majeruhi aliingia dakika
ya 75 kuchukua nafasi ya mgiriki Nikolaos Karelis aliyekuwa kwafunga
goli la kwanza la Genk, ushindi huo wa KRC Genk unakuja ikiwa ni
baada ya kukubali kipigo cha goli 3-2 katika mchezo wa kwanza ugenini
dhidi ya Rapid Wien, Genk sasa watacheza mchezo wao wa tatu
October 20 dhidi ya Athletic Bilbao ya Hispania