.

.

Ijumaa, 30 Septemba 2016

Hatimae Man United wapata ushindi wa kwanza Europa League


Baada ya kuanza vibaya kwa klabu ya Man United katika mchezo wake wa
kwanza waEuropa League dhidi ya Feyenoord nchini Uholanzi, usiku
wa Septemba 29 Man United walishuka tena dimbani kucheza mchezo
wao wa pili wa Kundi A Europa Leaguedhidi ya Zorya.
38eee44600000578-3814356-image-a-90_1475181520619
Man United ambao mchezo wa kwanza walipoteza kwa goli
1-0 dhidi ya Feyenoordambao walikuwa na rekodi ya kushinda mechi
nane mfululizo, wamecheza mchezo wao wa pili wa Europa League
dhidi ya Zorya katika uwanja wao wa Old Trafford na kufanikiwa kushinda
kwa goli 1-0 lililofungwa na Zlatan Ibrahimovic dakika ya 69.
38eee11f00000578-3814356-image-a-87_1475181251503
Kufuatia ushindi huo  Man United wanakuwa nafasi ya tatu katika
msimamo wa Kundi A linaloongozwa na Fenerbahce aliyepata
ushindi wa kwanza wa Europa League leo dhidi ya Feyenoord na
kuivunjia rekodi yao ya kucheza mechi 9 bila kufungwa
 nafasi ya pili wakiwa Feyenoord na Zorya wakishika mkia kwa
kusalia na point moja, Man Unitedwatacheza mchezo
wao wa tatu dhidi ya Fenerbahce October 20 2016.
38ef2a3700000578-3814356-image-a-21_1475183714544