.

.

Ijumaa, 16 Septemba 2016

MATUKIO MBALIMBALI BUNGENI WAZIRI MKUU AKILIAHIRISHA BUNGE MPAKA NOVEMBA 1, 2016


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa
 akilihutubia Bunge kabla ya kutoa kauli ya kuliahirisha bunge hilo mpaka
 tarehe 1 Novemba 2016 ambapo mbali na mambo mengine amesema serikali itaendelea kutekeleza yale iliyoyaahidi na kuwashukuru wadau mbalimbali
wanaoendelea kujitolea kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi
mkoani Kagera, wakati wa kikao cha nane cha Bunge la kumi na moja la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania


Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wakiimba wimbo wa taifa
baada ya Waziri Mkuu kuliahirisha Bunge hilo mpaka
tarehe 1 Novemba 2016, Leo Mjini Dodoma.


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Job Ndugai akitoka katika ukumbi wa Bunge baada ya Waziri Mkuu
kuliahirisha Bunge hilo mpaka tarehe 1 Novemba 2016, Leo Mjini Dodoma


Baadhi ya Wabunge wakibadishana mawazo na Waziri Mkuu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa baada ya kuliahirisha
Bunge hilo mpaka tarehe 1 Novemba 2016, Leo Mjini Dodoma


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye
akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Ubungo Mhe. Said Kubenea,
baada ya Waziri Mkuu kuliahirisha Bunge hilo mpaka
tarehe 1 Novemba 2016, Leo Mjini Dodoma.