IBRAHIM AJIBU
Masaa yanahesabika kuelekea mchezo wa Simba dhidi ya Azam. Lakini pamoja na mchezo huo kusubiriwa kwa hamu imeleta mashaka kwa wapenzi wa Simba sababu mshambuliaji Ibrahim Ajib amezua hofu ya kuwepo kwenye mchezo huo.
Ajib aliumia mazoezi baada ya kugongana na Novatus Lufunga wakati wakigombania mpira katika mazoezi yaliyofanyika Boko Veteran. Jambo kubwa lililozua hofu kwa mashabiki wa Simba ni kuona Ajib akishindwa kuendelea huku mguu wake wa kushoto akiwa amefungwa Bandeji.
