.

.

Alhamisi, 22 Septemba 2016

Aika aeleza furaha ya Navy Kenzo kutajwa kwenye MTV MAMA 2016

aika
Kwa Navy Kenzo, kutajwa kuwania kipengele cha kundi bora kwenye tuzo za mwaka huu ni ishara kuwa wamefika pazuri na kama wakiishinda kabisa, huo utakuwa ni mwanzo wa vitu vikubwa zaidi.
“Tumepata furaha sana maana inaonyesha kwamba kipaji chetu na ubunifu wetu umetambulika Afrika nzima,” Aika ameiambia Bongo5.


“Magroup ni mengi na sisi kuwekwa kwenye vitengo na legends kama wale inaonyesha juhudi na investments tulizoweka zimeanza kurudisha maana, furaha yetu ni pale mtu anapotambua kazi yetu,” ameongeza.
_mg_0780
Aika anadai kuwa kutajwa kwao kumekuja kama surprise lakini pia walitarajia makubwa mwaka huu. “This time tulifanya kazi kwa kusema lazima Tanzania iwepo kwenye hii category ya best group,” anasema.
Kuhusu kazi mpya, Aika amesema, “Video mpya ipo tayari, ila tukitoka coke studio wiki ijayo tunaenda South Africa kushoot ile video nyingine na Alikiba.”