.

.

Ijumaa, 27 Januari 2017

MAONYESHO YA WASANII WA TANZANIA YAANZA NAIROBI

Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Bi. Talha Mohamed Waziri (kulia) akimkaribisha Balozi wa Msumbiji kwenye maonesho hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa maonesho wa Village Market Nairobi nchini Kenya.

Ofisa wa Ubalozi wa Venezuela Nairobi, Jose Gregorio Ayila Torres (katikati) akibadilishana mawazo na Kaimu Balozi wa Tanzania (kulia). Kushoto ni mmoja wa wasanii wa Tanzania, Raza Mohamed.

Raia wa Uswisi waliofika kwenye maonesho wakijadiliana jambo wakati wa maonesho hayo yaliyoshirikisha wasanii 14 kutoka Tanzania wa uchoraji yaliyoanza toka juzi katika ukumbi wa maonesho wa Village Market Nairobi.

Wapenda sanaa wa Kenya wakikagua kazi za wasanii wa Tanzania kwenye ukumbi wa maonesho wa Village Market Nairobi.

Wadau wa sanaa wakifurahia maonesho yaliyowakutanisha Wasanii wa sanaa ya uchoraji 14 kutoka Tanzania huku yakihudhuliwa na wadau mbalimbali kutoka nchini Kenya