.

.

Jumanne, 6 Desemba 2016

MWANASIASA MKUU WA UPINZANI NCHINI GAMBIA AACHIWA HURU

media
Mwanasasa mkuu wa upinzani nchini Gambia Ousseynou Darboe mwaka 2011.
Nchini Gambia, mwanasiasa mkuu wa upinzani Ousseynou Darboe ameachiwa kwa dhamana Jumatatu wiki hii. Kesi yake ambayo iko katika ngazi ya rufaa imechukua mwelekeo ambao haukua unatarajiwa baada ya ushindi wa Adama Barrow katika uchaguzi wa urais.
Kiongozi wa chama cha UDP (United Democratic Party) alikuwa mmoja wa wanasiasa wakuu wa upinzani kwa utawala wa Yahya Jammeh. Alihukumiwa mwezi Julai kifungo cha miaka mitatu jela, kwa kosa la kuandaa na kufanya maandamano kinyume cha sheria na kesi yake katika ngazi ya rufaa yake imeanza Jumatatu wiki hii.
Ousseynou Darboe hivi karibuni ameachiwa kwa dhamana. Majaji wa mahakama ya rufaa tayari wametangaza kuachiwa kwake kwa dhamana. Alihukumiwa na watu kumi na nane katika chumba kidogo cha mahakama, huku wakisaidiwa na wanasheria kumi na tano. Kesi katika ngazi ya rufaa ilianza saa 4:00 asubuhi, lakini tatizo ni kuwa wanasheria wa serikali ya Gambia hawakuepo. Walikuja wakichelewa dakika kumi na tano, lakini waliomba radhi. Kulikua na watu wengi katika mji, na foleni ilikua ndefu, wanasheria wa serikali walisema.
Wanasheria wanaomsaidia Ousseynou Darboe na wafuasi wengine wa chama chake cha UDP, walitaja hali ya kipekee kwa sasa: "ushindi wa muungano wa upinzani katika uchaguzi wa urais wiki iliyopita". Ni kwa maslahi ya wote ambao wataachiwa huru, alisema mwanasheria. Hata ikiwezekana waachiwe kwa dhamana, mwanasheria huyo aliongeza. Mwanasheria mwengine alisema watu hawa wanaohukumiwa leo ni viongozi wa muungano, wako madarakani. Katiba inaamuru kuwa serikali inapaswa kuundwa tarehe 18 Januari 2017. Hali ya sasa, wakiwa gerezani haiwaruhusu kutekekeza majukumu yao.
Wakili wa Serikali, hakusema chochote wakati wa kesi hiyo ilipokua ikisikilizwa. Alikataa kueleza chochote na kusema mara tatu: mahakama ndio itachukua uamuzi.