.

.

Jumatatu, 28 Novemba 2016

ZIARA YA MAKONDA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI KINONDONI YANOGA

TUCHAPE KAZI KIONGOZI: Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akimwaga kicheko na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya mkoa huo, walipokuwa wkijadili jambo, baada ya kuzungumza na viongozi na watendaji kutoka wilaya ya Kinondoni, katika Bwalo na Maofisa wa Polisi, Msaki mwanzoni mwa ziara yake katika mkoa wa Dar es Salaam, jana. Zifuatazo ni taswira katika picha kama alivyowanasa Mmiliki wa theNkoromo Blog, Bashir Nkoromo aliyekuwa katika ziara hiyo.






 TANDALE

 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikagua chumba cha biashara cha Mamalishe (kushoto), aliyemkuta akiwa kazini eneo la Tandale, akiwa katika ziara ya kusikiliza kero za wananchi
Makonda akimwangalia mamalishe huyo wakati akiandaa chakula 
 Makonda na msafara wake wakikatiza mitaa ya Tandale wakati akisaka kero za wananchi wakati wa ziara hiyo ya aina yake. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Salum Ali Hapi, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida na wanne ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro.

Salum Ali Hapi akimpa maelezo Makonda walipofika kukagua eneo maarufu kwa jina la Uwanja wa Fisi, lililopo Tandale, Kata ya Manzese

Makonda akizungumza na wateja wa pombe za kieyeji aliowakuta katika kwenye kilabu cha pombe hizo, eneo la Uwanja wa Fisi

Jamaa aliyejitambulisha kwa jina la Mandela akikata funda la pombe ya kienyeji mbele ya Makonda bila wasiwasi kuwa yupo na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam.

SOURCE, MJENGWA