.

.

Jumamosi, 29 Oktoba 2016

SIMBA SC YAENDELEZA UBABE LIGI KUU, YAWAPIGA 3-0 MWADUI KAMBARAGE KICHUYA AFIKISHA GOLI 8.


Na Mwandishi Wetu, SHINYANGA

SIMBA SC imezidi kupiga kasi kuelekea kwenye taji la ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya jioni ya leo kuichapa Mwadui FC mabao 3-0 Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
Ushindi huo unaifanya timu ya kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog icheze mechi 12 za Ligi Kuu msimu huu bila kupoteza, ikishinda 10 na kutoa sare mbili.
Aidha, matokeo hayo yanaifanya Simba SC ijinafasi kileleni mwa Ligi Kuu kwa kufikisha pointi 32, mbele ya mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 24 za mechi 11.