Luis Suarez amezua hofu kwa mashabiki wa timu ya taifa ya Uruguay na Barcelona baada ya kuonekana amepata majeruhi kufuatia kugongana na mchezaji mwenzake, Diego Godin wakiwa mazoezini ambapo Suarez alikuwa akicheza kama golikipa. Kuelekea kwenye mchezo wa kufuzu kwa fainali za kombe la dunia dhidi ya Colombia huko jijini Barranquilla
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29 aliamua kuvaa gloves na kucheza kama golikipa kwenye mazoezi ambapo aligongana na Godin wakiwa kwenye harakati za kuwania mpira na kumsababishia maumivu makali ambayo yalimuweka chini kwa muda mrefu
Hata hivyo wachezaji wenzao hawakuonekana kujali baada ya wawili hao kuanguka chini na kugugumia kwa maumivu.
Uruguay ambao wanaongoza kwenye msimamo wa kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 kwa bara la Amerika Kusini, wamesafiri hadi jijini Barranquilla kuvaana na Colombia ambao wapo kwenye nafasi ya nne huku Brazil nao wakielekea huko Merida kupambana na Venezuela wanaoshika nafasi ya mwisho
Kama Brazil wakishinda halafu Uruguay wakashindwa kushinda, basi mabingwa hao wa dunia mara tano watatoka nafasi ya sita waliyopo sasa hadi nafasi ya kwanza wakiwa wamecheza mechi nne tu chini ya meneja mpya, Adenor Bacchi maarufu kama Tite.



