Mwanaharakati wa Tanzania wa kupinga ndoa za utotoni, Rebeca Gyumi ambaye
ni Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali, Msichana Initiative linalotetea
haki za wasichana kupata elimu ameshinda tuzo ya umoja wa Mataifa inayotolewa
kupitia UNICEF katika kipengele cha mabadiliko ya kijamii.
Mwanzoni mwa mwaka 2016 Rebeca Gyumi kupitia kwa wakili Jebra Kambole
wa Law Guards Advocates, walipinga kifungu cha 13 na 17 vya sheria
ya ndoa kinachoruhusu mtoto wa kike kuolewa akiwa na miaka 14 kwa
kibali cha mahakama, na miaka 15 kwa ridhaa ya wazazi.

July 08 2016 Mahakama Kuu ilitoa hukumu ikikubali kwamba vifungu hivi vya
sheria ya ndoa vinapingana na katiba ya nchi kwa kuweka umri tofauti wa
kuoa/kuolewa kati ya mtoto wa kike na wa kiume. Mahakama pia iliitaka
serikali kupitia kwa Mwanasheria Mkuu kujipanga ili kuvirekebisha vipengele
hivi tata ndani ya mwaka mmoja.