.

.

Alhamisi, 15 Septemba 2016

Phil Jones kuwa nje ya uwanja kwa mwezi mmoja


                                                                 Phil Jones


Beki wa klabu ya Manchester United, Phil Jones anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa muda wa mwezi mmoja kutokana na matatizo ya goti aliyoyapata akiwa mazoezini.
Kocha wa timu hiyo Jose Mourinho amethibitisha kuhusu tatizo hilo na kusema kuwa uchunguzi unaendelea.
Jones amekuwa akiandamwa na majeraha ya mara kwa mara na ni mchezaji ambaye amekuwa na uwezo wa kucheza kama beki wa kati, pembeni na mara kadhaa kama kiungo mkabaji.