Chelsea waliochini ya kocha wao Antonio Conte wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani walikubali kufungwa goli 2-1 dhidi ya vijana wa Jurgen Klopp, Chelseawalichukua dakika 19 kuruhusu magoli mawili yaliowafanya wakose point tatu wakiwa nyumbani, Dejan Lovren ndio alianza kupachika goli la Liverpool dakika ya 17.
Wakati Chelsea wanatafakari namna ya kusawazisha Jordan Henderson akapachika goli la pili dakika ya 36, goli pekee la Chelsea lilifungwa na Diego Costa dakika ya 62, hii ni mara ya pili mfululizo kwa Chelsea kuruhusu kufungwa na Liverpool katika uwanja wake wa nyumbani kwa mechi za Ligi Kuu.
Msimamo wa EPL baada ya mchezo huo